• Author
  Posts
 • #813

  Mabula Emmanuel
  Keymaster

  Na Mabula emmanuel
  0783676690
  Kijambua ni nini? neno kujitambua linatokana na neno tambua lenye maaana ya kujua ukweli wa kitu Fulani kwa kina,kwahiyo kujitambua ni hali ya kujijijua vilivyo kwa kina.ingawa watu wengi sana waishi lakini hawajitambui kaw kina.

  Huwezi kuzungumzia ujasiriamali bila kumtaja Mungu. Lakini pia huwezi kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio bila ya kujitambua. Wakati huo huo huwezi kujitambua bila ya kumjua Mungu vizuri, kujitambua ninakozungumzia ni tafsiri pana zaidi yenye maana zaidi ya kujua wewe ni jinsi gani? Una rangi gani nyeusi au nyeupe? Kabila gani? Umezaliwa wapi? Na lini? Na nyingine nyingi zinazofanana na hizo.
  Tafsiri ya kujitambua ninayoizungumzia ni ile yenye kumaanisha kujua kwanini ulizaliwa? Umekuja hapa duniani kufanya nini? Umetokea wapi na unaenda wapi?
  Je? Umewahi jiuliza kuwa kabla hujazaliwa na mama yako mzazi ulikuwa wapi? Yaani kabla ya miezi tisa,ulikokuwa kuna fananaje? Kuna mandhari gani? Je! Kunwafanana na Mwanza, Mbeya Dar es salaam, Marekani, Paris unapata picha yeyote ya mahali ulipo kuwa kabla ya kuzaliwa?.
  Lakini pia umewahi kujiuliza kwa nini upo hapa duniani? Yaani kwa nini unaishi? Thamani yako juu ya huu ulimwengu unaijua? Yaani uwepo wako unajua una thamani gani? Katika maisha ya watu wengine na dunia kwa ujumla na kwanini ulizaliwa kabla ya ukoloni au baada ya ukoloni? Kwanini ulizaliwa afrika na si kwingineko,Unaweza ukawa hujui kwanini ulizaliwa na kwanini unaishi lakini je? Unajua unaenda wapi yaani unakujua unapokwenda kuna fananaje?
  Umewahi kujiuliza maswali kama haya hata kabla ya kuwaza kufanya biashara gani? Katika maisha ya mafanikio ni lazima sio ombi kuwa ili uweo kufanikiwa katika kiwango kikubwa ni lazma uwe umeyapata majibu ya masali ya hapo juu. Kwamba kama unafanya biashara basi iwe ni biashara inayotokana na kipaji chako ndipo utakapopata mafanikio makubwa. Amini usiamini matajiri (watu wenye mafanikio) duniani kote wanajua kwanini walizaliwa kwanini wanaishi lakini pia wanajua wanakokwenda. Kwahiyo ili ufanikiwe ni lazima ujue umetoka wapi? Na unakwenda wapi? Na kwanini upo hapa duniani.kwa mfano umewahi kuona nguo au viatu vinavyozalishwa na kampuni ya bhaharesa,jibu ni hapana kwani hata nguo zilizopo ni jezi tu ya timu anayomiliki lakini zaidi ya hapo hakuna kwa maana ya aina nyingine ya mavazi kama vile nguo za kina baba ,mashati, suluali nguo za kina mama na watoto na biashara nyingine nyingi, je Unadhani kwa utajiri alionao hawezi kuzifanya?.siri kubwa ambayo wewe hujui ni kwamba bhaharesa ANAJUA KWANINI ALIZALIWA.nikweli bakresa anajua kwanini alizaliwa ndo maana anajua kwanini yupo hapa duniani na anajua anakokwenda,bakresa aligundua yupo hapa duniani kwaajiri ya kuwalisha watu tu,huduma anayoifanya ni ya vyakula na vinywaji tu. pamoja na kwamba anafanya na mambo mengine lakini huduma yake kubwa ni chakula.kwa mfano uwepo wa timu unamwongezea masoko na uwepo wa azam logistic unamuongezea urahisi katika usafirishaji wa huduma yake ya chakula ndani ya nchi na nje ya nchi.mfano mwingine ni Mengi mkurugenzi wa IPP MIDEA.mMengi ni mmoja pia ya watanzania wenye mafanikio na ni mfano wa kuigwa.lakini pia Mengi nae kama bakresa aligundua kwanini yupo hapa duniani ambapo aligundua yupo hapa kwaajiri ya kuwahabarisha watanzania.uthibitisho wa hili ni uwepo wa magazeti,vituo vya redio,vituo vya runinga kama vile.ITV,EATV.RADIO ONE,EARADIO,CAPITAL,NIPASHE,THE GURDIAN.mifano ipo mingi sana lakini hawa ni baaadhi tu,ukweli utabaki palepale kuwa huwezi kufika kokote bila kujua unakwenda wapi na bila kujua ulikotoka na kwanini upo hapo ulipo baadhi ya waliofanikiwa kujua walikuja hapa duniani bila kujali wamezaliwa wapi.
  Ndo maana katika jamii nyingi katika mataifa mbali mbali duniani ikiwemo na nchi yangu Tanzania, ambayo raia wake wamekuwa wakiilalamikia Serikali zilizo madarakani kuwa haziwajiri kwani zimewatenga na kusababisha maisha kuwa magumu sana siku hadi siku. Ni ukweli usiopingika kuwa “Serikali inasehemu yake katika kuhakikisha Taifa lina kuwa na maendeleo lakini pia mtu binafsi nae anasehemu yake katika kuhakikisha kuwa yeye binafsi anakuwa na maendeleo na Taifa lake kwa ujumla.
  Kwa mfano unajua ni kwanini walio nje ya ajira wanalalamika kuwa maisha ni magumu kwa sababu wamekosa ajira, walio ndani ya ajira wanalalamika kuwa maisha ni magumu kwa sababu mishahara haitoshi, inaishia kulipa kodi, ada za watoto na mambo mengine mwisho wa siku wanabaki na akiba ndogo sana ambayo hawasaidi kufanya chochote, lakini pia wapo waliostafu pia na wao wanalalamika kuwa maisha ni magumu sana kwani hawana tena ajira wanasubiria ela ya pensheni inayotoka kila baada ya miezi kadhaa kwa mazingira kama hayo inawawia vigumu kwa waliowengi kuishi maisha yasiyomagumu.yote haya yanatokea ni kwasasababu watu wengi tangu wakiwa wadogo hawajui kwanini wapo hapa duniani,wametoka wapi na wanaenda wapi,ndo maana utakuta mtu anafanya biashara aina tofauti nyingi akidhani ndo ujanja kumbe anajidanganya.hivyo ukiweza kijibu maswari niliyo yauliza hapo awali,tayari wewe ni tajiri. Hatakama umesoma sana bila kujua kwanini upo hapa duniani,wewe ni bure. baadhi ya wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu je? Wangapi wanajua kwanini wapo hapa duniani na wanajiandaaje kufikissha kalama zao kwa jamii kwa elimu walizozipata badala ya kulalamikia serikari kwa kila jambo.inawezekana kabisa serikari isiwe na kosa lolote ikitokea hujui upo hapo ulipo kufanya nini.
  Mambo makubwa mawili yanayosababisha watu waishi maisha magumu (umasikini uliokithiri).
  (a) Hawajijui Watu wengi wanaishi maisha magumu sana, moja ya sababu inayochangia kwa kiasi kikubwa watu wengi waishi maisha kimasikini ni kutojijua vema kwanini yupo hapa duniani, kauubwa ili afanye ni? Pia anataka afike wapi? Kwa sababu hawajijui mara nyingi wamekuwa ni watu wa lawama sana, lawana hizi zinapelekwa kwa Serikali iliyo madarakani hata sehemu iliyondani ya uwezo wao hawakosi lawama kwa ndugu utamsikia mtu akisema “Huyu ni ndugu yangu lakini hanijari hata kidogo na ana uwezo balaa” Wakati huohuo
  anaishi kwake, sasa mtu kama huyu anajijua kweli je! Anatambua thamani yake. Na ndo maana mtu mmoja unamkuta akitoa lawama kwa ndugu, rafiki, Serikali na kitu chochote kitakachomzunga utasikia mti huu hauzai matunda,na njaa inauma. wakati mti ulipohitaji mahitaji yake yeye hakutimiza mahitaji kama vile kumwagilia maji, mbolea au palizi.Lakini inapofika msimu wa mavuno na mti umedumaa bado anaendelea kutoa lawama kwa mti.
  Kumbe swala la kujitambua kiundani ni jambo la kwanza kabisa kabla haujachukua hatua ya kufanya kitu chochote. Pamoja na kwamba kwa mujibu wa dini yako umefundisha kuwa upo hapo duniani ili kumtumikia Mungu hilo ni sahihi kabisa,lakini je ni kwa kutoa huduma gani kwa jamii inayokuzunguka? Je? Ni huduma ya usafiri shaji,chakula,mavazi,ujenzi n.k
  Neno biashara kwa maneno mengine pia tunaweza kusema huduma. Kwa mfano biashara ya nguo na viatu unapokuwa unaifanya katika jamii Fulani kwa maneno mengine tunaweza kusema unatoa huduma ya mavazi kwa jamii. Mchungaji, Shehe, Maimamu, Askofu, Ustadhi na viongozi wengine wa dini wao kwa pamoja wanatoa huduma ya Kiroho kwa jamii na mifano mengine mingi.
  Neno huduma ndani yake kuna biashara inafanyika na ndani ya biashara kuna huduma itolewayo Na hakuna huduma iliyomuhimu kuliko zote, zote zinategemeana. Ingawa watu wengi wanadhani huduma zitolewazo na wachungaji au mashehe na viongozi wa dini ni muhimu zaidi na za kimungu sana kuliko nyingine kitu ambacho si kweli, kama hilo ni kweli jaribu kufikiria kama watu wanao uza nguo au wanaotoa huduma ya mavazi kwa jamii wakigoma kutoa huduma hiyo kwa mdai kwamba jamii haitambui mchango wao, kwani jamii inadhani huduma zitolewazo na viongozi wa dini ni muhimu zaidi kuliko sisi hivyo tumeungana duniani kote hatupo tayari kutoa huduma zetu, swali la kujiuliza je? Wachungaji au
  mashehe pamoja na waumini zao wanaweza wakasali au kuswali wakiwa uchi wa mnyama yaani watupu kabisa wabaki kama walivyozaliwa? Jibu ni hapana huo utakuwa ni uwendawazimu. Kwa hiyo kila kitu kina umuhimu sawa hakuna kilicho juu ya kingine. Hivyo unatakiwa kutoa huduma kwa kujua umuhimu wako hautofautiani na mchungaji au shehe katika jamii yako wote mna umuhimu sawa mbele ya jamii, kama vile utafikaje msikitini, kanisani bila ya huduma ya usafiri kuwepo, lakini pia utafanyaje biashara bila ya kuwa na imani imara itakayokuwezesha kibiashara kufanikiwa ambapo huduma hizo hutolewa kanisani au misikitini ama sehemu inayofanana na hiyo.
  Kwa hiyo ili ufanikiwe kimaisha ni lazima ujitambue kiundani yaani mambo yafuatayo:-

  Tambua kuwa kwanini ulizaliwa yaani ulizaliwa ili ufanye kitu gani utoe huduma gani ama biashara gani kama ni huduma ya mavazi, basi iwe ni mavazi tu, kama ni siasa basi iwe siasa tu kama ni utangazaji basi iwe utangazaji tu, kama uchungaji basi iwe ni uchungaji tu usichanganye na kitu kingine.
  Wapo watu wanaodhani kufanya mambo mengi ndo njia rahisi ya wao kuwa na maisha mazuri kitu ambacho si cha kweli kwani kila mtu amepewa kalama ya pekee ambayo akifanikiwa kugundua kuwa yeye binafsi ana kitu gani akawekeza kwa bidii katika kalama yake bila shaka maisha yake yatakuwa ni yenye mafanikio.

  Tambua pia kwanini umezaliwa kabla au baada ya ukoloni kwa sababu kuna umuhimu wa kutambua hilo. Kwa mfano Mwl JK Nyerere alizaliwa kipindi cha ukoloni. Bahati nzuri aliweza kutambua kuwa yupo hapa duniani ili afanye nini na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuyatimiza yale aliyokuwa anapaswa kuyafanya ingawa kunaweza kukawa na dosari za hapa na pale.

  Kumbe kuzaliwa mda Fulani (msimu Fulani) inamaanisha kitu, kwa mfano huo wa Nyerere utagundua changamoto zilizokuwepo kipindi hicho zinatofautiana sana na changamoto wanazokumbana nazo wanasiasa wa leo. Hivyo kama siasa si kalama yako bali umelazimisha tu kwa sababu ya tamaa ya kuitwa mheshimiwa ni lazima ukwame. na uheshimiwa haupatikani kwa njia ya siasa tu,ndo maana kuna wanina Mengi,bakresa na wengine wengi pia na wao wanaitwa waheshiwa.kumbuka mshimiwa utaitwa kwa yale ulio yafanya nasi si kwasababu tu umechaguliwa na wananchi

  Kwa hiyo fahamu ya kuwa kuzaliwa nyakati Fulani kuna maana si bure. Kila nyakati zinachangamoto zake. Hivyo baada ya kujua umezaliwa ili ufanye kitu gani pia swala la kutambua kuwa kwanini ulizaliwa nyakati hizo ulizozaliwa ni jambo la msingi sana kulitambua.kwani Mungu anakusudi maalumu unadhani kwanini haukuzaliwa mwaka 1920 jibu ni kwamba umezaliwa mwaka uliozaliwa kwa sababu maalum hivyo inakupasa utambue hilo ili uweze kufanikiwa. na huo ndio ujasliamali kweli.neno ujasiliamali limaanishe kufanya ulicho umbiwa ktk kiwango cha juu sana kama baadhi ya wajasilimali nilio wataja yaani uwe na ujasili wa kufanya kile ulicho kigundua kipo ndani yako.

You must be logged in to reply to this topic.