• Author
  Posts
 • #778

  Mabula Emmanuel
  Keymaster

  Makala haya yanalenga kuchambua kwa kina tabia za wajasiriamali, na kukusaidia kutathmini tabia zako dhidi ya tabia za kijasiriamali na namna ya kujijengea tabia hizi.Dhumuni likiwa ni kujitambua na kujiendeleza mwenyewe tayari kwa fani ya ujasiriamali.

  A: Tabia za Wajasiriamali
  Tabia tano (5) za kumtambua mjasiriamali
  Tabia 1: Hamu ya kufanikiwa.
  Tabia 2: Tabia ya kujitegemea na kuwa na uhuru wa kujitawala.
  Tabia 3: Tabia ya ubunifu na uvumbuzi.
  Tabia 4: Tabia ya kuthubutu kuchukua hatari ya kadiri na iliyotathminiwa.
  Tabia 5: Msukumo na nia ya dhati ya kusimama katika lengo.
  B: Jinsi ya kujipima kama una tabia kuu za kijasiriamali (Jaribio la TAZAKI) TAZAKI ni kifupi cha TAbia ZA KIjasiriamali.Jaribio la TAZAKI linapima tabia binafsi zinazopatikana kwa watu wajasiriamali.Tabia hizi zinajumuisha:Hamu ya kufanikiwa; Kujitegemea na kuwa na uhuru wa kujitawala; tabia ya ubunifu na uvumbuzi; kuthubutu kuchukua hatari na msukumo wa ndani na nia dhabiti ya kusimama katika lengo.Jaribio hili lilitengenezwa na kuhakikiwa kufuatia utafiti uliofanywa ukiangazia aina mbalimbali ya vipimo vinavyotumika katika kutathmini ujasiriamali na biashara na ni kazi iliyofanywa na Sally Caird katika shule ya biashara ya chuo kikuu cha Durham. Namna ya kutumia jaribio la TAZAKI katika kujitambua kama una tabia za kijasiriamali.Jibu kama unakubaliana(K) au haukubaliani(S) na sentensi 54 zilizoorodheshwa hapa chini.Sentensi hizi zimepewa namba kuanzia 1 hadi 54 na namba hizi zimeonyeshwa katika gridi ya shiti ya majibu.Kwa kila namba iliyopo katika shiti ya majibu izungushie (K) kama unakubaliana na sentensi hiyo au (S) kama hukubaliani nayo.Usifikirie muda mrefu kuhusiana na jibu.Sasa unaweza kuanza.
  C: Zifuatazo ni sentensi 54 za kujipima kama una tabia za kijasiriamali
  1. Mimi sitajali kama kazi ninayoifanya ni ya kawaida na isiyokuwa na changamoto endapo malipo ni mazuri.
  2. Wakati ninapoweka lengo langu mwenyewe la kitu chochote naweka lengo lenye ugumu kufikika.
  3. Sipendelei kufanya vitu vipya au visivyofuata desturi na taratibu.
  4. Watu hodari,stadi,wenye akili wanaoshindwa kuwa na mafanikio hawakuchukua fursa wakati zilipojitokeza.
  5. Mara chache nasongwa na mawazo ya vitu visivyo dhahiri.
  6. Mara zote natetea mtazamo wangu binafsi kama kuna mtu hakubaliani na mimi.
  7. Ninaamini kuwa kwa asili mtu anafanikiwa kwasababu ana kipaji katika jambo fulani na juhudi hazichangii kwenye mafanikio hayo.
  8. Mara nyingine watu wanaona mawazo yangu sio ya kawaida.
  9. Kama ningepewa shilingi 1000 kwa ajili ya kucheza kamari ningenunua tiketi ya bahati na sibu kuliko kucheza karata.
  10. Ninapenda changamoto ambazo zinazidisha uwezo wangu kuliko vitu ambavyo naweza kuvifanya kirahisi.
  11. Ningalipendelea kuwa na kipato cha kawaida katika kazi ambayo nina uhakika wa kudumu nayo kuliko katika kazi ambayo ina kipato kikubwa ambayo naweza kuipoteza wakati wowote kama utendaji wangu sio mzuri.
  12. Napendelea kufanya vitu katika njia yangu mwenyewe bila kuhofia watu wengine wanafikiria nini. 13. Mengi ya maisha magumu yanayowakabili watu ni kutokana na kutokuwa na bahati katika maisha. 14. Napendelea kufuatilia vitu hata kama inamaanisha kukabiliana na matatizo wakati wa kufanya hivyo. 15. Kama kuna vikwazo na mojawapo ya kazi zangu za siku,naiacha na kuanza kufanya kazi nyingine.
  16. Ninapoweka mipango ya kufanya kitu fulani,karibia mara zote ninafanya ninachokipanga
  17. Sipendelei mabadiliko ya ghafla katika maisha yangu
  18. Nitathubutu kuchukua hatari kama nafasi ya kufanikiwa ni 50 kwa 50.
  19. Nafikiria zaidi wakati uliopo na uliopita kuliko wakati ujao.
  20. Kama ningelikuwa na wazo zuri la kutengeneza fedha ningalikuwa tayari kukopa kiasi cha fedha inisaidie kulitekeleza.
  21. Wakati nikiwa katika kikundi ninafurahia kuachia mtu mwingine aongoze.
  22. Kimsingi watu wanapata kile wanachostahili 23. Sipendelei kufanya kitu mpaka kuwepo na taarifa za kutosha.
  24. Ni muhimu zaidi kufanya kazi vizuri kuliko kujaribu kuwafurahisha watu
  25. Nitapata ninachokitaka kama nitawafurahisha watu walio na mamlaka kuliko mimi.
  26. Watu wengine wananiona kama mtu mwenye kuuliza maswali mengi.
  27. Kama kungeonekana dalili za kushindikana kwa kitu basi ni afadhali nisingalikifanya hicho kitu.
  28. Ninakasirishwa kama watu hawajali muda.
  29. Kabla sijafanya uamuzi ninapenda kutafiti kila kitu haijalishi ni muda gani itanichukua
  30. Wakati naifanya kazi yangu ni mara chache sana nahitaji au nataka msaada.
  31. Mafanikio hayaji mpaka unapokuwa eneo muafaka na katika muda muafaka.
  32. Napendelea kuwa na uelewa wa vitu kadhaa kuliko kuwa na uelewa wa ndani sana wa kitu kimoja tu. 33. Ningependa kufanya kazi na rafiki yangu,hata kama sio mchapakazi, kuliko kufanya kazi na mtu nisiyemjua na kumpenda ambaye ni mzuri sana kikazi.
  34. Mafanikio ni matokeo ya kufanya kazi kwa bidii,hayahusiani kwa namna yoyote na bahati.
  35. Napendelea kufanya vitu katika njia za kawaida mara nyingi kwa mazoea kuliko kujaribu kufanya vitu katika njia mpya na tofauti.
  36. Kabla sijafanya uamuzi muhimu,napendelea kupima faida na hasara kuliko kutumia muda mwingi kufikiria kuhusiana na suala lenyewe.
  37. Ni heri ningefanya kazi kama mshirika katika timu kuliko kufanya mwenyewe
  38. Ningetumia fursa ambayo ingenipelekea kwenye mambo mazuri zaidi kuliko kufurahia kufanya mambo kwa mazoea.
  39. Ninafanya kile kinachotegemewa kutoka kwangu,na kufuata mwongozo.
  40. Kwangu mimi, kupata kile ninachokitaka suala la kubahatisha halina nafasi.
  41. Napenda kuishi kwa mpangilio ili maisha yaweze kwenda bila bugudha na kwa mujibu wa mpango. 42. Wakati nakabiliwa na changamoto nafikiria zaidi kuhusiana na matokeo ya kufanikiwa kuliko athari za kushindwa.
  43. Ninaamini kwamba yanayonitokea mimi katika maisha kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na watu wengine.
  44. Nina uwezo wa kushughulika na mambo mengi kwa wakati mmoja
  45. Naona ugumu kuomba fadhila kutoka kwa watu wengine
  46. Naamka mapema,nabaki kazini muda mrefu au napitiliza milo ili kuhakikisha kazi maalum za kipaumbele zinafanyika.
  47. Kile nilichokizoea mara zote ndio bora kwangu kuliko mambo mapya.
  48. Watu wengi wanafikiri mimi ni mkaidi.
  49. Kushindwa kwa watu mara chache sana ni matokeo ya maamuzi yao mabovu
  50. Mara nyingine nakuwa na mawazo mengi ya biashara sijui ni lipi la kuchagua.
  51. Kwangu ni rahisi kupumzika siku za mapumziko.
  52. Napata ninachokitaka kutoka kwenye maisha kwasababu nafanya kazi kwa bidii kuvitafuta.
  53. Ni vigumu sana kwangu kuendana na mabadiliko kuliko kufuata desturi.
  54. Napenda kuanzisha miradi mipya ambayo inaweza kuwa na hatari ya kushindwa

You must be logged in to reply to this topic.