• Author
  Posts
 • #819

  Mabula Emmanuel
  Keymaster

  1. MAMBO YA JUMLA YA KUZINGATIA.
  1.1. Mtu yeyote anayedhamiria kufanya biashara ya chakula kwa matumizi ya binadamu sharti atume maombi TFDA kwa ajili ya usajili wa majengo na kibali cha kuendeshea biashara hiyo.

  1.2. Ili kutimiza matakwa ya kisheria,mwombaji ana wajibu kufuatilia maelekezo kwa ajili ya usajili wa majengo ya utengenezaji bidhaa za chakula na leseni ya biashara. Maelekezo haya yanapatikana kutoka kwa maafisa afya wa wilaya(DMO’s),Ofisi za kanda za TFDA,Makao makuu ya TFDA,au kupitia tovuti ya TFDA ambayo ni http://www.tfda.or.tz.

  1.3. Majengo na biashara ya chakula vitajumuisha yafuatayo:
  i. Utengenezaji wa bidhaa za chakula.Hii inamaanisha Majengo ambapo operesheni zinazojumuisha uzalishaji,usindikaji,ujazaji na ufungashaji zitafanyika..
  ii. Uhifadhi na Uuzaji wa bidhaa za chakula.Hii inamaanisha mahali chakula kitahifadhiwa,kuuzwa,kusambazwa au kutangazwa.

  1.4. Malipo ya ada sharti yafanyike kupitia mkurugenzi wa Mji/ Wilaya/Manispaa/Jiji waliopo nchi nzima au kupitia akaunti namba 2041100069, NMB, tawi la Kariakoo kwa akaunti ya shillingi na akaunti namba 02J1021399100, CRDB,tawi la Holland house, Dar es Salaam,kwa akaunti ya fedha za kigeni.Makato yote ya benki yatabebwa na mwombaji.
  1.5. Taarifa zote na mawasiliano kuhusiana na maombi yatafanyika aidha kwa Kiingereza au Kiswahili.

  2.0. VITU MAALUM VYA KUZINGATIA.
  2.1. Kwa utengenezaji wa bidhaa za chakula,fomu ya maombi sharti ijumuishe.

  (i).Fomu za maombi zilizojazwa kwa ajili ya usajili wa majengo na leseni.
  (ii).Chati inayoonyesha mtiririko wa mchakato wa utengenezaji wa bidhaa husika.
  (iii) Mpangilio wa Kiwanda.
  (iv) Cheti cha mtu mwenye ujuzi na shughuli husika.
  (v) Barua kutoka kwa mtu mwenye ujuzi akikiri kuwa tayari kusimamia utengenezaji wa bidhaa husika.

  2.2. Kwa uhifadhi na Uuzaji wa bidhaa za chakula.Mwombaji sharti apeleke fomu za maombi zilizojazwa kwa ajili ya usajili wa majengo na leseni

  3.0 JINSI YA KUFANYA MAOMBI KWA AJILI YA USAJILI WA MAJENGO NA KIBALI CHA BIASHARA.
  3.1. Maombi yote kwa ajili ya usajili wa majengo na Kibali cha kuendesha biashara ya chakula sharti yafanywe kwa Mkurugenzi mkuu wa TFDA kupitia fomu ya usajili wa majengo (TFDA No.1) na kwa ajili ya leseni ya biashara kupitia fomu namba (TFDA No.3).
  3.2. Maombi sharti yakusanywe makao makuu ya TFDA/Ofisi za kanda au kupitia wakurugenzi wa halmashauri za wilaya/ manispaa/jiji ambapo biashara ilipo.
  3.3. Baada ya kupokea maombi yaliyokamilika na malipo ya ada stahili kama inavyoainishwa katika kanuni ya mwaka 2011 inayoongoza ada na makato katika chakula,madawa na vipodozi Tanzania.mwombaji atapokea risiti ya malipo.
  3.4. Mipango,dizaini,na ujenzi wa majengo sharti uende sambamba na kanuni ya mwaka 2006.
  3.5. Mwombaji anashauriwa kutafuta ushauri kutoka kwenye ofisi za mamlaka ili kukidhi matakwa ya kanuni ya mwaka 2006 ya usafi wa chakula pamoja na mambo mengine.
  3.6.Wakati ujenzi au ukarabati umekamilika,mkaguzi sharti atafanya ukaguzi wa kina wa awali kabla ya usajili kwa kutumia checklist ya biashara husika na kutoa maoni na mapendekezo kuhusiana na ubora wa majengo katika fomu ya maombi.
  3.7. Katika maeneo ambapo ofisi za TFDA zipo kama vile TFDA Makao makuu au ofisi za kanda,ukaguzi utafanyika kwa pamoja kati ya mkaguzi kutoka TFDA pamoja na mkaguzi wa chakula anayeteuliwa kutoka serikali za mitaa.
  3.8. Wakaguzi watahakikisha kuwa taarifa zote zilizopo kwenye checklist zimejazwa kikamilifu,kusainiwa na kupigwa muhuri na wote,yaani mwombaji na Mkaguzi.

  3.9. Baada ya kupokea fomu za maombi,checklist ya ukaguzi,na dokyumenti muhimu kutoka serikali za mitaa na ofisi zetu za kanda,Mkurugenzi mkuu atazipitia fomu zote na kuthibitisha kuzipokea..
  3.10. Mkurugenzi mkuu anaweza kupitisha,kushikilia au kukataa maombi yeyote na kutoa sababu kwa uamuzi wake wa kukataa au kushikilia.
  3.11.Kwa watengenezaji wa bidhaa za chakula ambao maombi yao ya usajili wa majengo yamekubalika,watapata barua ya maelekezo ikiwataka kuzalisha sampuli ya bidhaa husika kwa ajili ya matumizi ya usajili wake.Baada ya kufanikiwa kusajili bidhaa,mwombaji atakabidhiwa cheti cha usajili wa jengo na kibali cha biashara.
  3.12. Waombaji ambao maombi yao yameshikiliwa kwa sababu yeyote ile watatakiwa kufanya marekebisho au kutoa maelezo ya kina ndani ya miezi sita ili kupitiwa tena.Baada ya kipindi hiki kumalizika,maombi yatakuwa yameondolewa.
  3.13.Mamlaka baada ya kujiridhisha kuwa jengo linakidhi matakwa ya kisheria,itatoa cheti cha usajili wa jengo na kibali cha biashara kwa Mwombaji.
  3.14. Maombi yote yanayoshughulika katika biashara za chakula zifuatazo yatachambuliwa na kama yatakidhi haja yatapitishwa na mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa/ jiji/Wilaya kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa TFDA
  i. Bucha
  ii. Maduka ya chakula ya reja reja
  iii. Migahawa iv. Hoteli
  v. Mashine za kusaga
  vi. Kantini and Kioski
  vii. Maduka ya chakula ya jumla
  ix. Wahudumiaji wa chakula katika matukio
  x. Nyumba za Machinjo
  xi. Wachuuzi wa chakula na
  xii. Baa.

You must be logged in to reply to this topic.